Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa tamko kufuatia mpango wa serikali kutangaza kusitisha urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Bunge kuanzia terehe 26.1.2016.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu amesema Chama cha Chadema kimekosa imani na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na matendo ya kidikteta na kwenda kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa kutaka kuminya uhuru wa wananchi wa kupata habari.
Akizungumzia matendo hayo amesema ni pamoja na kuzuia Shirikia la Utangazaji la Tanzania(TBC), kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya bunge inayoendelea ,kufutwa kwa Gazeti la Mawio pasipo kuwa na sababu za msingi, kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara pamoja na kuunda kamati dhaifu bungeni.
Amesema kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye ametoa sababu zisizokuwa za msingi akidai kuwa serikali inaepuka gharama za kurusha matangazo hayo moja kwa moja na baadala yake kurekodi vikao hivyo vya bunge kwa kurushwa saa nne usiku
Amesisitiza kuwa Waziri Nape hajafanya utafiti na kwamba ikiwa tatizo lipo kwenye gharama alizotaja chadema ipo tayari kuchangia gharama hizo kwa kuanzisha harambee maalumu pamoja kuwataka chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari (Moat) na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT) kulisimamia suala hilo.
Akizungumzia Kamati za Bunge amesema serikali imeunda kamati dhaifu bungeni kwa nia ya kudhoofisha shughuli za utendaji bungeni na maendeleo ya nchi kwa kuwaweka wabunge wageni kwenye kamati muhimu ilhali hawana uwezo kuzisimamia.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment