Na Wolter John, Babati
Wakazi wa kijiji cha matufa kitongoji cha Burunge
kata ya magugu Wilaya ya Babati mkoani manyara wameingiwa hofu kubwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa ambao haujafahamika mpaka sasa.
Akizungumza
na Mwandishi wa Blog hii mwenyekiti
wa kijiji cha cha burunge kata ya matufa, Ramadhan Mangi ameeleza kuwa mpaka sasa
ugonjwa huo haujafahamika na umeua watu wawili wa familia moja huku
wengine watano wakiwa bado wanaendelea na matibabu katika kituo cha afya cha
Magugu.
Asha Shabani
ni mmoja ya waathirika wa ugonjwa huo na
ambaye pia baba yake amefariki kutokana
na ugonjwa huo ameeleza kuwa alianza kujisikia vibaya na kukosa hamu ya kula na baada ya muda kidogo alianza kutapika, kuharisha na alipopelekwa hospitali alitibiwa
na alipotaka kujua anaugua ugonjwa gani daktari hakuweza kumjibu.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa kitongoji cha Burunge Dismas Baranda amesema kuwa ugonjwa mpaka sasa una muda wa wiki
mbili na kila mgonjwa anapoenda kupima huambiwa ni homa ya matumbo kitu ambacho
kinaleta hofu kubwa kutokana na ugonjwa huo kuendelea kusambaa kwa wengine.
Madaktari wa
kituo cha afya magugu wamewaeleza
wakazi hao hawana maabara ya kuweza
kupima na hivyo wamepeleka vipimo katika
maabara ya hospital ya mkoa ya Arusha
ya Mount Meru kwa ajili ya kupata majibu.
Hata hivyo wakazi
hao wameshauriwa kutumia maji safi yaliyochemshwa, kula vyakula vya
moto,kutoshikana mikono, kuchimba matundu ya vyoo pamoja na kuwapatia vidonge
maalum ili kujikinga na ugonjwa huo.
Post a Comment