HATIMAYE shindano la kumsaka mrembo alibino jijini Mwanza limefikia tamati baada
ya ZAWADI Dotto (17) kuibuka kidedea na kutawazwa kuwa mshindi katika shindano
hilo baada ya kuwagaragaza wapinzani wake sita.
Shindano hilo lililofanyika juzi usiku jijini hapa huku likiwakutanisha
wasichana saba wenye ualbino ili kumpata mshindi
atakaye wakilisha Mkoa kitaifa.
Warembo hao Hajra Sadru, Furaha Elias, Zabibu Abdalah, Anthonia
Mathias,Pendo Faustine na Asteria Christopher walionyesha madaha na ubunifu jukwaani
wakisaka nafasi hiyo.

Hata hivyo walioingia tatu bora katika mpambano huo ni
Zawadi Dotto, Furaha Elias
na Hajra Sadru,ambapo Dotto aliweza kung’ara zaidi na kuwaacha wawili
hao.
na Hajra Sadru,ambapo Dotto aliweza kung’ara zaidi na kuwaacha wawili
hao.
Mara Baada ya Zawadi Dotto kutangazwa mshindi, alisema kuwa hakuamini
kama angeweza kushika taji hilo na kuahidi kuwa atahakikisha
anasimamia haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.
Pia aliwashauri walemavu wa ngozi kujitokeza kugombea nafasi za
mbalimbali za uongozi ili kuleta usawa kwenye jamii na kuitaka
serikali kutoa fursa kwa maalbino.
“Kwakeli sikutarajia kama ningeweza kushinda taji hili,kwasababu wote
umewaona walivyo safi,mimi nakiri kuwa ni kudra za Mungu labda nitapambana
kupigania haki za watu wa Albino”alisema Dotto
Mlimbwende huyo aliweza kujinyakulia zawadi ya Simu aina ya Solar
5,kitita cha Sh 100,000 na Godoro,huku mshindi wa pili Hajra Furaha simu,godoro na Sh 80,000 na watatu simu,godoro na Sh 50,000.
Mwisho
Post a Comment