Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya
Mrisho Kikwete, ameteuliwa kuwa mjumbe mpya wa umoja wa Afrika AU kwenda
nchini libya akichukua nafasi ya Mohamed Dileita aliyeshika nafasi hiyo
tangu mwaka 2014.
Uteuzi huo uliofanywa na Umoja wa Afrika
katika kikao chake kilichofanyika jijini Addis Ababa nchini Ethopia
kimeleza uteuzi huo ni sehemu ya juhudi za umoja huo kuhikisha usalama
unarudi nchini libya.
Kamishina wa Amani na usalama wa
AU,Smail Chergui jana alitangaza uteuzi huo alipokuwa anatoa muhtasari
wa majadiliano na makubaliano ya kikao hicho kilichiwakutanisha viongozi
wa ngazi za juu wa nchi wanachama.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment