Na Sheila Sezzy
Zaidi ya wakazi 1000 wakiwemo wanawake wenye rika tofauti
pamoja na vijana wa kiume waliokuwa wakijihusisha na biashara ya ngono na
matumizi ya madawa ya kulevya jijini hapa wameachana na vitendo hivyo baada ya
kupatiwa elimu juu ya athari za ngono isiyo salama pamoja na matumizi ya madawa
ya kulevya.
Elimu hiyo imetolewa na ya shirika lisilo la kiserikali linalo saidia makundi ya watu walio hatarini kuambikizwa magonjwa ya ukimwi na kifua kikuu (ICUP) wakishirikiana na wadau mbalimbali jijini hapa lengo likiwa ni kuokoa makundi ya watu walio katika mazingira hatarishi.
Elimu hiyo imetolewa na ya shirika lisilo la kiserikali linalo saidia makundi ya watu walio hatarini kuambikizwa magonjwa ya ukimwi na kifua kikuu (ICUP) wakishirikiana na wadau mbalimbali jijini hapa lengo likiwa ni kuokoa makundi ya watu walio katika mazingira hatarishi.
Akiongea na Raia Tanzania jana wakati wa mkutano wa wadau wa robo mwaka wa kujadili maendeleo ya mradi huo wa utoaji wa elimu kwa makundi hayo meneja mradi wa ICUP, Azizi Itaka alisema kuwa katika kipindi cha miezi 6 wameweza kuwaokoa watu zaidi ya 1000 kwa kuwatumia waelimishaji rika ambao awali walikuwa wakijihusisha na biashara ya ngono na madawa ya kulevya.
Itika alisema kuwa baada ya kutoa elimu kwa watu wanaofanya vitendo hivyo wale ambao wanakuwa tayari kubadilika wanapelekwa katika vituo vya afya kwa ajili ya kupima afya zao na baadae kupatiwa dawa za kupunguza makali ya VVU pamoja na kupatiwa mipira kwa ajili ya kujikinga na maambukizi mapya.
“Dhana ya kuwa kutoa dawa na kuwapatia kondomu ni kuwahamasisha kuendelea na biashara hiyo sio kweli kwasababu tunachokifanya ni kuilinda jamii ambayo wanaishi nayo”alisema Itaka.
Alisema kuwa katika mradi huo wamekumbana na changamoto nyingi ikiwemo ya askari kuwakamata waelimisha rika wao wanapokuwa kazini nyakati tofauti wakidhani kuwa na wao ni moja ya madada poa au vijana wanaobugia na kujidunga madawa ya kulevya.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa mkoa Jemes Kengia alisema kuwa sasa hivi maambukizi ya VVU mkoani Mwanza yameshuka hadi kufikia asilimia 4.2 na kudai kuwa kuanzishwa kwa mradi huo kutachangia maambukizi hayo kushuka zaidi.
Kwa upande Devotha Johanes aliyekuwa mfanyabiashara wa ngono kabla ya kubadirika na kuwa muelimisha rika alisema kuwa wakati alipokuwa akifanya biashara ya kuuza mwili alikuwa akishi maisha ya shida kutokana na kuleweshwa pombe kupita kiasi na kupigwa na wahuni na wakati mwingine alibwakwa.
“Kuna mambo mengi yaliyokuwa yakisababishwa kupigwa moja ni ile ya kudai malipo baada ya kutumikia ngono,kuna wakati nilikuwa napatiwa lakini wakati mwingine nilikuwa sipatiwi”alisema Devotha.
Alisema kuwa sasa hivi anaishi maisha ya raha na anawashauri akina dada kuachana na biashara hiyo sababu siyo salama kwa maisha yao kutokana nakuwa katika hatari ya maambukizi ya VVU.
Licha ya maambukizi ya Ukimwi kutajwa kupungua hadi kufikia asilimia 4.2 mkoani Mwanza , biashara ya ngono imetajwa kukua na kutishia kuongezeka kwa maambukizi VVU hivyo jitihada zinatakiwa kuongezeka ili kukabiliana na hatari hiyo.
Post a Comment