Kumekuwa na mapigano usiku kucha
katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya
kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza.
Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao,na kwamba udhibiti wan chi uko mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo ,Bujumbura.
Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga .mwandishi wa BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa.
Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment