vote

Mpinzani wa Rais Museveni kuitikisa Uganda akitokea Ulaya

Taharuki Kampala kufuatia habari kuwa Mpinzani wa rais Museveni anarejea leo kutoka Ulaya.



Taharuki imetanda mjini Kampala Uganda baada ya habari kuenea kuwa mpinzani mkuu wa rais Yoweri Museveni ,aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi anarejea leo.

Inadaiwa kuwa  polisi wametumwa katika barabara ya kutoka Kampala hadi kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe.

Bwana Mbabazi anasemekana kuwa anarejea kutoka kwa ziara ya kimataifa iliyompeleka Uingereza na Marekani huku wafuasi wake wamepanga kumkaribisha kwa shangwe na vigelegele.

Pamoja na msafara wa magari yaliyojaa wafuasi wake kumkaribisha.

Amama Mbabazi alitangaza majuma mawili nia ya kushindana na rais Museveni kuwania uwenyekiti wa chama cha National Resistance Movement na hatimaye kuwania kiti cha urais.

Chanzo: Hivi Sasa
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog