BARAZA la
wazee la Kata ya Magu mjini, Kitongosima na Lumeji lenye Jumla ya wazee 150,
limeiomba serikali itungie sheria sera ya wazee ya mwaka 2003.
Pia
wameomba kutengewa chumba chao maalumu kwaajili ya matibabu katika
zahanati, vituo vya Afya,Hospitali za Wilaya,mikoani na Hospitali za Rufaa
nchini.
Wakizungumza
na uongozi wa shirika la MAPERECE kupitia viongozi wa mabaraza wazee hao
walieleza kuwa, sera ya wazee imekaa mda mrefu bila kutungiwa sheria na hivyo
kuwa fanya wazee kukosa maamuzi yakudai haki zao kama ilivyo ainishwa katika
sera ya wazee ya mwaka 2003.
Hermenegid Mganga, ni Katibu wa Balaza la wazee kata ya
Magu mjini ambaye alieleza kuwa kuwepo kwa sheria hiyo, kutawasaidia wazee
kupata haki zao bila kuwa na matatizo yoyote katika upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa
wazee.
Angizungumzia
suala la Afya kwa wazee, Mganga aliiomba serikali kutenga vyumba vya matibabu
kwaajili ya waze kutokana na baadhi ya wilaya kutotekeleza huduma za matibabu bure kwa wazee.
“sisi kama
wazee, tunaiomba serikali itutengee na sisi vyumba maalumu kama
walivyotengewa wanawake wajawazito na
kliniki za watoto ili tupate huduma za Afya kwa utaratibu unao faa” Alisema
Mganga.
Hata hivyo alieleza
kuwa, katika kuhakikisha hilo, ni vema serikali ikatambua umuhimu wa
miundombinu na huduma za Afya kwa wazee na kuziboresha kwani vituo vingi havina sehemu ya kusubilia matibabu na kwamba
wanapofika katika vituo huhitaji sehemu ya kukaa na kupumzika wakisubilia
huduma.
Post a Comment