![]() |
Hizi ni baadhi ya dawa zilizokamatwa nyumbani kwa Mtuhumiwa huyo |
MAMLAKA ya chakula na dawa nchini TFDA kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi nchini limekamata dawa zenye thamani ya Milioni 97 zenye uzito
wa tani 42 zilizokuwa zikimilikiwa kinyume na taratibu za umiliki wa
dawa.
Dawa hizo aina 127 zimekamatwa juzi nyumbani kwa Charles Mbusiro
Mkoani Mwanza baada ya uchunguzi uliofanywa na mamlaka hiyo na
kugundua kuna jengo kubwa nyumbani kwake alilokuwa akihifadhia dawa
hizo ambalo halikuwa na sifa za kuhifadhi dawa kisheria.
![]() |
Meneja usalama wa dawa TFDA, Kissa Mwamwitwa akizungumza na mwandishi wa blog hii. |
chakula na dawa, Kissa Mwamwitwa alisema kuwa jjengo hilo lilikuwa na
dawa bandia, zilizokwasha muda, zilizopigwa marufuku na nyingine
ambazo hazijasajiliwa na TFDA.
“ Hii ni baada ya kuona chimbuko la dawa bandia limekuwa likitokea
Kanda ya ziwa, wengi tuliokuwa tukiwakamata na dawa bandia walikuwa
wakidai kuwa wamenunua katika duka la dawa la Mbusiro ndipo tukaanza
uchunguzi bila mafanikio” alisema Mwamwitwa.
![]() |
Meneja ysalama TFDA Kissa Mwamwitwa akipiga hesabu ya Dawa zilizokamatwa. |
Mwamwitwa alisema kuwa baada ya kuchunguza duka la mmiliki huyo na
kutokuwepo kwa dawa bandia, waliamua kutumia uchunguzi wa kina kwa
kushirikiana na wananchi ndipo walipogundua jengo hilo lililopo
nyumbani kwake Ilemela.
“mwanzo alileta ugumu kufungua jengo hilo lakini baada ya kumuelewesha
alifungua ndipo tukaingia na kukuta dawa hizo ambazo ni mali ya
Tanzania,Uganda na Kenya” alisema Mwamwitwa.
Mwamwitwa alisema kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kufungua mlango aliweka
ngazi nyuma ya nyumba kisha kuruka na kutokomea kusikojulikana huku
akidai kuwa mujibu wa sheria ya baraza la duka la dawa nchini
atanyang’anywa leseni ya biashara ya dawa.
Baadhi ya Dawa alizokamatwa nazo Mtuhumiwa huyo ni za kutibu Tb,
malaria, Antibiotic na dawa za kuongeza nguvu za kiume.
Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi, Obadia Jonas
kutoka makao makuu alisema kuwa wataendelea kumsaka mtuhumiwa huyo kwa
ajili ya kujibu tuhuma hizi.
“Ameruka ukuta kwa kutumia ngazi, lakini hiyo ni presha tuu,
tutaendelea kumtafuta ili aweze kujibu shitaka”. Alisema Jonas
Post a Comment