vote

KOPUNOVIC AWAPA SIMBA SC HADI IJUMAA KUAMUA HATIMA YAKE, POPPE ASEMA…





HATIMA ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic (pichani juu) kuendelea au kutoendelea na kazi Simba SC itajulikana Ijumaa.

Hiyo inafuatia mwalimu huyo kipenzi cha wana Simba kuuambia uongozi wa klabu hiyo kwamba atawapa jibu Ijumaa.

Goran ameshindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Simba SC juu ya Mkataba mpya, kutokana na kutaka kiwango cha fedha ambacho klabu imeona ni kikubwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba Kopunovic ametaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000 (Sh. Milioni 16).

“Sisi tumempa ofa yetu, ambayo ameikataa. Sasa amesema anakwenda kwao kwa mapumziko, akiwa huko, Ijumaa atatoa jibu. Nasi tutamsikilizia hadi hiyo Ijumaa,”amesema Poppe.

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba iwapo hawatafikia makubaliano na Kopunovic basi watatafuta kocha mwingine.

Goran ameiongoza Simba SC katika mechi 24 tangu aanze kazi Januari mwaka huu kati ya hizo, timu imeshinda mechi 18, sare mbili na kufungwa nne.

Source. Bin Zubery
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog