vote

Wakimbizi 8000 wakwama baharini

Wakimbizi wakwama baharini karibu na Thailand

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM, linasema kuwa maelfu ya wakimbizi kutoka Bangladesh na Myanmar, wamekwama baharini karibu na Thailand baada na kushindwa kufika ardhini.

Msemaji wa IOM aliiambia BBC kuwa hatua za hivi majuzi za kukabiliana na wahamiaji haramu kutoka jamii ya Rohingya ina maana kuwa walanguzi hawawezi kuwafikisha ardhini wahamiaji na sasa karibu watu 8,000 wemekwama kwenye mashua.

Katika siku mbili zilizopita, zaidi ya wakimbizi 100 walifika nchini Malaysia na Mynmar.

Waandishi wanasema kuwa wahamiaji hao ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wauzwe na baadaye wazuiliwe kwa fidia na watu wanaofanya biashara haramu ya watu nchini Thailand.

Chanzo: BBC Swahili
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog