Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho akiambatana na Makatibu na walinzi wa Baraza hilo. |
Baraza la Wawakilishi Zanzibari linatarajia kukutana siku ya jumatano mei 13 kujadili Bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka fedha wa 2015/2016.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Wawakilishi Yahya Khamis Hamad amesema kwamba Wajumbe wa Baraza hilo watapata nafasi ya kujadili Bajeti hiyo ambayo ndio mwelekeo mzima wa shughuli zote za kiserikali. Katika mkutano huo jumla ya maswali 81 yataulizwa na kujibiwa.
Ameongeza kuwa fursa hiyo ni muhimu kwa wajumbe hao kuitumia vyema kujadili mambo ya msingi yanayowahusu wananchi badala kujadili mambo yasiyo na tija kwa wananchi.
Kwa upande mwingine Yahya amesema katika kikao hicho pia Miswada miwili ya sheria itawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo mswada wa Sheria ya Fedha na Mswada wa sheria wa kuidhinisha matumzi ya serikali kwa mwaka 2015/2016.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment