Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiongea na Madereva kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dares salaam. |
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo( CHADEMA) Freeman Mbowe amewasili kituo kikuu cha Mabasi Ubungo kwa lengo la kukutana na Madereva waliogoma kwa shinikizo la serikali kutatua kero zao mbalimbali zinazokabili ikiwemo kutakiwa kwenda kusoma.
Mara baada ya kuwasili Ubungo madereva pamoja na wananchi wamemlaki kwa shangwe huku wengine wakifagia barabara pamoja na kuimba nyimbo mbalimbali suala lilipekelea shughuli zote za kibiashara kusimama kwa masaa kadhaa.
Aidha, naye mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda aliyewasili katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo amewaomba madereva kuendelea na kazi na kuwahidi kuyafanyika kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi kesho.
Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa, ambayo itajadili masuala ya mikataba, malipo, matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao.
Kwa upande mwingine Madereva hao wamekubali maombi hayo na kuanza safari kwa sharti la kutaka kusikilizwa kero zao katika muda waliokubaliana.
Mara baada ya kupewa ahadi ya kupata majibu ndani ya siku saba, madereva hao wameanza safari katika maeneo mbalimbali hususani mikoa ya jirani kama Morogoro. Daladala nazo kuanzia majira ya saa kumi zimemiminika barabarani na kuanza kutoa huduma ya usafiri.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment