![]() |
Rais wa TFF Jamali Malinzi |
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ameitakia kila la kheri timu ya Young
Africans katika mchezo wake wa jumamosi wa Kombe la Shirikisho barani
Afrika (CC) dhidi ya timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia, mechi
itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake kwa klabu ya
Young Africans, Rais Malinzi amewaambia wanapaswa kupambana na
kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo wa jumamosi, ili kujiweka
katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano
kwani ndio pekee kwa sasa wanaoipeperusha bendera ya Tanzania katika
michuano ya kimataifa.
Young Africans imeingia katika
hatua ya 16 bora Kombe l Shirikisho barani Afrika,baada ya kuzitoa BDF
XI ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao (3-2), kisha
kuwaondoa FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza kwa jumla ya
mabao (5-2).
Endapo timu ya Young Africans
itafanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburia kucheza mechi ya
mtoano (Play-off) dhidi ya timu mojawapo zitakaotolewa katika 16 bora ya
Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).
Post a Comment