Wananchi wa Mwanza walalamika kuhusu kutopanda kwa nauli za daladala
BAADHI ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza wameilalamikia mamlaka ya usafiri nchi kavu na majini (Sumatra) kugoma kushusha nauli za daladala kwa kisingizio cha uendeshaji wa gharama kuwa kubwa ukilinganisha na za mafuta.
Hatua hiyo imekuja baada ya siku moja mamlaka hiyo kutangaza kushusha nauli za mabasi huku za daladala zikibaki pale pale hivyo kuwaumiza wananchi walio wengi kulingana na maisha yalivyo magumu.
Akizungumza na Blog hii mmoja wananchi hao Melisa Daudi Mkazi wa Ilemela alisema,mamlaka hiyo haikuwa makini na kwamba suala hilo huenda imeshinikizwa na wizara husika kwani tangu mafuta yashushwe hakukuwa na tamko lolte juu ya ushushwaji wa nauli.
“Mamlaka haina ilicho kifanya bali ni kutuumiza sisi kwa sababu tangu mafuta yashushwe kulikuwa hakuna tamko lolote ukilinganisha na muda ambao mafuta yakipanda kesho yake nauli zitapanda hivyo mimi naona huenda itakuwa imeshinikizwa na wizara husika ya mamlaka hiyo”alilalamika Melisa.
Aidha kwa upande wake Zuberi Mfinanga Mjasiriamali makoroboi alisema kuwa iweje mabasi yashushwe gharama za usafirishaji na kwamba daladala ziliendelee kuwa na nauli ile ile kitu ambacho bado kinawaumiza.
“mimi naona mabasi yanatumia mafuta ndio maana wameshusha lakini kwa daladala yanatumia maji ya ziwa victoria ndio maana hawajashusha,kwa sababu kama zote zinatumia mafuta kwa nini wasishushe alafu wakisingizia kikokotozi cha nauli hakikutoa ghrama halisi mbona yanapopanda kikokotozi kinatoa muda huohuo?’’alihoji Mfinanga.
Hata hivyo Mwanfunzi wa shule ya msingi kirumba Vailent Fredy mkazi wa Kiloleli alisema serikali haijamsaidia isipokuwa imeangalia kwa baadhi ya makundi ambao watanufaika na gharama hiyo licha ya kwamba haijashushwa.
“Mimi naishi kiloleli alafu nasoma Kirumba kwa maana hiyo napanda gari mbili kila siku natumia Sh 800 kwa hiyo kama serikali ingepunguza wakafanya Sh.100 ingetusaidia sana”alisema Vailent
Labels:
habari
Post a Comment