vote
Featured Post Today
print this page
Latest Post
Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Miss albino Mwanza Apatikana


HATIMAYE shindano la kumsaka mrembo  alibino jijini Mwanza limefikia tamati baada ya ZAWADI Dotto (17) kuibuka kidedea na kutawazwa kuwa mshindi katika shindano hilo baada ya kuwagaragaza wapinzani wake sita.

Shindano hilo lililofanyika juzi usiku jijini hapa huku likiwakutanisha
wasichana saba wenye ualbino ili kumpata mshindi
atakaye wakilisha Mkoa kitaifa.

Warembo hao Hajra Sadru, Furaha Elias, Zabibu Abdalah, Anthonia
Mathias,Pendo Faustine na Asteria Christopher walionyesha madaha na ubunifu jukwaani
wakisaka nafasi hiyo.
Hata hivyo walioingia tatu bora katika mpambano huo ni Zawadi Dotto, Furaha Elias
na Hajra Sadru,ambapo Dotto aliweza kung’ara zaidi na kuwaacha wawili
hao.



Mara Baada ya Zawadi Dotto kutangazwa mshindi, alisema kuwa hakuamini
kama angeweza kushika taji hilo na kuahidi kuwa atahakikisha
anasimamia haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.

Pia aliwashauri walemavu wa ngozi kujitokeza kugombea nafasi za
mbalimbali za uongozi ili kuleta usawa kwenye jamii na kuitaka
serikali kutoa fursa kwa maalbino.

“Kwakeli sikutarajia kama ningeweza kushinda taji hili,kwasababu wote
umewaona walivyo safi,mimi nakiri kuwa ni kudra za Mungu labda nitapambana
kupigania haki za watu wa Albino”alisema Dotto

Mlimbwende huyo aliweza kujinyakulia zawadi ya Simu aina ya Solar
5,kitita cha Sh 100,000 na Godoro,huku mshindi wa pili Hajra Furaha simu,godoro na Sh 80,000  na watatu simu,godoro na Sh 50,000.
Mwisho
0 comments

Coastal Union eye league glory under Mayanja







TANGA-BASED Mainland top flight side Coastal Union are
convinced that they can challenge for title after bringing in
Ugandan coach Jackson Mayanja.

The 1988 Tanzania champions have hired the former Uganda
midfielder Mayanja from Kagera Sugar, who finished a place
below them in the recently concluded season.

Coastal Union finished sixth on the log with 34 points; two
above Kagera Sugar but in Mayanja; they see a coach that will
see them perform better.

Union vice-chairman Steven Mguto is optimistic that
Mayanja’s enormous coaching experience will help improve
their team next season as they seek to return to glory days.

Mguto said the former Bunamwaya (now Vipers), URA FC, KCC
FC and Kiyovu trainer, has signed a two-year deal and will be
assisted by Joseph Lazaro.

He added that Union have also taken measures to strengthen
their squad after recruiting striker Abasarim Chidiebere from
Stand United on a one-year contract. “We have also promoted
players from our second string side.

They are Mtenje Albano, Tumaini Karim, Mohamed Shekue
and Fikirini Suleiman,” Mguto revealed.

Coastal Union spokesperson Oscar Assenga backed Mguto’s
sentiment saying the club has set its target on winning the top
flight silverware and that is the reason they have hired the
new coach.

On his side, Mayanja said he was happy to join Coastal Union
and was looking to a successful career with the Tanga outfit.

He said he wants to steer the team to domestic and
international successes and urged Coastal leaders and
members to unite and support their team
0 comments

MKATABA WA MESSI HAUJACHAKACHULIWA

Add caption




KLABU ya Simba imekanusha tuhuma za kuuchakachua mkataba wa winga wake, Ramadhani Singano 'Messi' kama anavyodai.



Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini hapa jana mchana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara, amesema klabu inatambua mkataba wa Messi wa miaka mitatu unaomalizika mwakani na si mwaka huu kama anavyodai winga huyo.



"Habari hizi ni upotoshwaji, Simba haijachezea mkataba wa Messi kutoka miaka miwili na kuwa mitatu, Messi ni mchezaji mdogo sana. Naambia hao mawakala uchwara, waache kumvuruga. Hii ndiyo staili yangu ya leo," amesema Manara.



"Tunaomba TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) walitolee ufafanuzi suala hili badala ya kukaa kimya kwa sababu taswira ya Simba inachafuka," amesema zaidi Manara aliyeonekana kufura kwa hasira.
Chanzo: Mpenja Blog
0 comments

Rais wa FIFA Sepp Blatter kujiuzulu


Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter


Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa atajiuzulu kama rais wa shirikisho hilo kufuatia kashfa ya ufisadi.

Akitangaza kujiuzulu,kwake Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mara moja ili kumchagua rais mpya.

Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi .

Lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu.Shirikisho la FIFA lilikumbwa na mgogoro wa kukamatwa kwa maafisa wake kutokana na mashtaka ya ufisadi ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa na marekani .

Uchunguzi mwengine unaofanywa na serikali ya Switzerland kuhusu vile michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 na 2022 ilitolewa pia unaendelea.''Nimehusika sana na FIFA na maslahi yake.Kilicho muhimu kwangu ni taasisi ya FIFA na Soka duniani''.

Chanzo: BBC Swahili
0 comments

FPCT: Vijana ibueni miradi ya maendeleo




WANACHI na wakazi  wa Jiji la Mwanza, wametakiwa kutotegemea serikali peke yake, badala yake kuongeze bidii katika kuhakikisha wanaibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi ili kukuza uchumi.

Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa Shirika Lisilo la kiserikali MWAOMI,  linalohudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na utunzaji wa Mazingira  Fredrick Eliakim alipokuwa akifungua maadhimisho ya sherehe ya  siku ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni 16 kila mwaka,

alieleza kuwa, serikali peke yake haitaweza kutekeleza mahitaji ya watanzania wote bila ya wananchi wenyewe na mashirika binafsi kuonesha umuhimu wao katika jamii inayo wazunguka.

“Serikali haiwezi kufanya kila kitu bali inahitaji kuungwa mkono na mashirika binafsi yenye uwezo kifedha katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa”alisema Eliyackimu.

Alieleza kuwa,shirika hilo lililoko chini ya uongozi wa  Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT),limekuwa na mchango mkubwa kwa serikali kupitia Nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na Elimu, Afya, na Utunzaji wa mazingira katika shule za msingi  zilizopo kata ya Buswelu wilayani Ilemela.

Sherehe hizo, znazofanyika jijini hapa katika uwanja wa shule ya msingi Kahama, zilishirikisha wadau mbalimbali wa Elimu wilayanmi humo ikiwa ni pamoja na walimu na wanafunzi kutoka katika shule nane ambazo ni Lukobe,Masemele,Kisabo, Igogwe, Nyamwilekelo, kahama na kabusungu, zote za kata ya Buswelu.

“Tumefanya sherehe hizi kwa kushirikiana na walimu wote lengo likiwa ni kuwajengea watoto kukua katika Nyanja mbalimblai ikiwa ni pamoja na Kijamii,Kisaikolojia, Kimwili,Kiakili na pia kihisia” alisema.


sambamba na hilo Maadhimisho hayo yaliambatana na michezo mbalimbali kutoka katika shule hizo, ikiwani njia moja wapo ya wanafunzi kudadilishana mawazo katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, mazingira na mambo mengine ya kuwajengea uwezo wanafunzi .

Afisa elimu na mzingira wilayani humo Benatus Kahulu aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa manispaa hiyo John wanga alisema aliupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kazi nzuri wanayo ifanya ya kuhakikisha inasaidia Jamii ya wana Ilemela bila kujali dini wala kabila.

 Mratibu wa idara ya Michezo kutoka katika Shirika la MWAOMI Dicksoni  Juma, alieleza kuwa, wameamua kuanza mashindano hayo mapema, ili kuwaandaa watoto vizuri na katika kuhakikisha siku hiyo wanaifikia wakiwa na furaha kutokana na ushirikiano uliopo wa shule hizo za msingi .

Alieleza kuwa kupitia mashindano hayo, Shirika limeandaa zawadi mbalimblai kwa washindi  ambazo watakabidhiwa Siku ya tarehe 16 Juni ambayo itakuwa ni siku ya mtoto wa Afrika Duniani, hivyo aliwataka walimu na wanafunzi kutoa ushirikiano wao wa dhati katika kuhakikisha sherehe hizo zinamalizika kwa amani na utulivu.

“sisi tumejipanga katika kuhakikisha mashindano haya yanakamilika kwa wakati muafaka, hivyo ni jukumu la walimu na wanafunzi wenyewe kuona umuhimu wa mashindano haya ambayo huleta umoja, ushindi na mshikamano baina yao”alisema Dickson.

shule zitakazoshiriki mashindano hayo kuwa ni pamoja na Lukobe,Masemele,Kisabo,Igogwe,Nyamwilekelo, Kahama, Kabusungu na ,Kilabela na  kwamba timu itakayo shinda katika kinyang’anyilo hicho, itapata zawadi ya Kombe, jezi na mpira kwa  mshindi wa kwanza, na mshindi wa pili na watatu watapata zawadi ya jezi na mpira.

Mashindano hayo, yalifunguliwa na mechi mbili kati ya shule ya msingi  Nyamwilolelwa na kabusungu, ambapo upande wa mpira wa miguu shule ya msingi nyamwilolewa  iliibuka  kidedea kwa bao 6-0 dhidi ya kabusungu huku mpira wa pete nyamwilolelwa ikishinda mabao 30 dhidi ya kabusungu ilioambulia bao 3. 





0 comments

KOPUNOVIC AWAPA SIMBA SC HADI IJUMAA KUAMUA HATIMA YAKE, POPPE ASEMA…





HATIMA ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic (pichani juu) kuendelea au kutoendelea na kazi Simba SC itajulikana Ijumaa.

Hiyo inafuatia mwalimu huyo kipenzi cha wana Simba kuuambia uongozi wa klabu hiyo kwamba atawapa jibu Ijumaa.

Goran ameshindwa kufikia makubaliano na uongozi wa Simba SC juu ya Mkataba mpya, kutokana na kutaka kiwango cha fedha ambacho klabu imeona ni kikubwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba Kopunovic ametaka dola za Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba na dola 8,000 (Sh. Milioni 16).

“Sisi tumempa ofa yetu, ambayo ameikataa. Sasa amesema anakwenda kwao kwa mapumziko, akiwa huko, Ijumaa atatoa jibu. Nasi tutamsikilizia hadi hiyo Ijumaa,”amesema Poppe.

Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba iwapo hawatafikia makubaliano na Kopunovic basi watatafuta kocha mwingine.

Goran ameiongoza Simba SC katika mechi 24 tangu aanze kazi Januari mwaka huu kati ya hizo, timu imeshinda mechi 18, sare mbili na kufungwa nne.

Source. Bin Zubery
0 comments

Ratiba ya hatua ya robo fainali klabu bingwa ulaya leo.

  1. Week 5
  2. Week 6
  3. Week 7
  4. Week 8
  5. Week 9
  6. Week 10
  7. Week 11
  8. Week 12
  9. Week 13
  10. Week 14
  11. Week 15
  12. Week 16
  13. Week 17
  14. Week 18
  15. Week 19
  16. Week 20
  17. Week 21

Jumanne, April 21

Bayern Munich
3:45 PM
Porto
Barcelona
3:45 PM
Paris SG

Jumatano, April 22

Monaco
3:45 PM
Juventus
Real Madrid
3:45 PM
Atlético Madrid
0 comments

Kikosi Cha Yanga kitakachokabiliana na Stand United Muda mfupi ujao.

kikosi cha Yanga


1.Deogratius Munishi "Dida"
2.Juma Abdul Mnyamani.
3.Oscar Fanuel Joshua.
4.Rajab Zahir.
5.Mbuyu Twite.
6.Juma Said Makapu
7.Simon Happygod Msuva.
8.Haruna Niyonzima "Fabregas"
9.Amiss Jocelyn Tambwe.
10.Mrisho Halfan Ngassa "Anko"
11.Andrey Coutinho.
BENCHI.
Ally Mustafa "Barthez"
Nizar Halfan
Pato Ngonyani
Hussein Javu
Kpah sean Sherman
Danny Mrwanda.
Kocha mkuu.
Hans Van Pluijm.
Msaidizi.
Charles Boniface Mkwasa "Master"
Meneja.
Hafidh Saleh.
0 comments

Etoile Du Sahel watua Dar: Waongozana na Rais wao, Bosi wa ‘FTF’ kuivaa Yanga Kesho






Wapinzani wa Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho
Afrika, Etoile du Sahel wamewasili jijini Dar es Salaam wakiwa tayari kabisa kuivaa Yanga kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho kimewasili na ndege ya Kampuni ya Nouvelair  BJ 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.

Wakiwa kwenye uwanja wa ndege wachezaji wa kikosi hicho cha Tunisia walionekana wako tayari kuivaa Yanga, kesho.

Msafara wao uliongozwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF), Krifa Jalel, akiwa na Rais wa Etoile du Sahel, Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10.

Taarifa zimeeleza Etoile itafikia katika Hoteli ya Ledger Plaza, zamani ikijulikana kwa jina la Bahari Beach eneo la Kunduchi, ambapo leo Ijumaa jioni inatarajiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini Msumbuji na wanatarajiwa kuwasili leo mchana, huku kamisaa wa mchezo huo, Salah Ahmed Mohamed kutokea nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote walitarajiwa kufikia katika Hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.



0 comments

Malinzi aitakia kila la kheri Yanga ikiivaa Etoile du Sahel.

Rais wa TFF Jamali Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ameitakia kila la kheri timu ya Young Africans katika mchezo wake wa jumamosi wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) dhidi ya timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar  es salaam.

Katika salamu zake kwa klabu ya Young Africans, Rais Malinzi amewaambia wanapaswa kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo wa jumamosi, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano kwani ndio pekee kwa sasa wanaoipeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya kimataifa.

Young Africans imeingia katika hatua ya 16 bora Kombe l Shirikisho barani Afrika,baada ya kuzitoa BDF XI ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao (3-2), kisha kuwaondoa FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao (5-2).

Endapo timu ya Young Africans itafanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburia kucheza  mechi ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu mojawapo zitakaotolewa katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).

 Source: Dauda

0 comments
 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog