WANACHI na wakazi wa Jiji la Mwanza, wametakiwa
kutotegemea serikali peke yake, badala yake kuongeze bidii katika
kuhakikisha wanaibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi ili
kukuza uchumi.
Wito huo umetolewa jana na Mratibu wa Shirika Lisilo la kiserikali MWAOMI, linalohudumia watoto
wanaoishi katika mazingira magumu na utunzaji wa Mazingira Fredrick Eliakim alipokuwa akifungua maadhimisho ya sherehe ya
siku ya mtoto wa Afrika ambayo hufanyika Juni 16 kila mwaka,
alieleza kuwa, serikali peke yake haitaweza kutekeleza mahitaji ya watanzania wote bila ya wananchi wenyewe na mashirika binafsi kuonesha umuhimu wao katika jamii inayo wazunguka.
“Serikali haiwezi kufanya kila kitu bali inahitaji kuungwa
mkono na mashirika binafsi yenye uwezo kifedha katika shughuli mbalimbali za
ujenzi wa Taifa”alisema Eliyackimu.
Alieleza kuwa,shirika hilo lililoko chini ya uongozi wa Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT),limekuwa
na mchango mkubwa kwa serikali kupitia Nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Elimu, Afya, na Utunzaji wa mazingira katika shule za msingi zilizopo kata ya Buswelu wilayani Ilemela.
Sherehe hizo, znazofanyika jijini hapa katika
uwanja wa
shule ya msingi Kahama, zilishirikisha wadau mbalimbali wa Elimu
wilayanmi humo
ikiwa ni pamoja na walimu na wanafunzi kutoka katika shule nane ambazo
ni Lukobe,Masemele,Kisabo, Igogwe, Nyamwilekelo, kahama na kabusungu,
zote za kata
ya Buswelu.
“Tumefanya sherehe hizi kwa kushirikiana na walimu wote
lengo likiwa ni kuwajengea watoto kukua katika Nyanja mbalimblai ikiwa ni
pamoja na Kijamii,Kisaikolojia, Kimwili,Kiakili na pia kihisia” alisema.
sambamba na hilo Maadhimisho hayo yaliambatana na michezo mbalimbali
kutoka katika shule hizo, ikiwani njia moja wapo ya wanafunzi
kudadilishana mawazo katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu,
mazingira na mambo mengine ya kuwajengea uwezo wanafunzi .
Afisa elimu na mzingira wilayani humo Benatus
Kahulu aliyemuwakilisha Mkurugenzi wa manispaa hiyo John wanga alisema
aliupongeza uongozi wa
shirika hilo kwa kazi nzuri wanayo ifanya ya kuhakikisha inasaidia Jamii
ya
wana Ilemela bila kujali dini wala kabila.
Mratibu wa idara ya Michezo
kutoka katika Shirika la MWAOMI Dicksoni Juma, alieleza kuwa, wameamua kuanza
mashindano hayo mapema, ili kuwaandaa watoto vizuri na katika kuhakikisha siku
hiyo wanaifikia wakiwa na furaha kutokana na ushirikiano uliopo wa shule hizo
za msingi .
Alieleza kuwa kupitia mashindano hayo, Shirika limeandaa
zawadi mbalimblai kwa washindi ambazo
watakabidhiwa Siku ya tarehe 16 Juni ambayo itakuwa ni siku ya mtoto wa Afrika
Duniani, hivyo aliwataka walimu na wanafunzi kutoa ushirikiano wao wa dhati
katika kuhakikisha sherehe hizo zinamalizika kwa amani na utulivu.
“sisi tumejipanga katika kuhakikisha mashindano haya
yanakamilika kwa wakati muafaka, hivyo ni jukumu la walimu na wanafunzi wenyewe
kuona umuhimu wa mashindano haya ambayo huleta umoja, ushindi na mshikamano
baina yao”alisema Dickson.
shule zitakazoshiriki mashindano hayo kuwa ni
pamoja na Lukobe,Masemele,Kisabo,Igogwe, Nyamwilekelo, Kahama, Kabusungu na ,Kilabela
na kwamba timu itakayo shinda katika
kinyang’anyilo hicho, itapata zawadi ya Kombe, jezi na mpira kwa mshindi wa kwanza, na mshindi wa pili na
watatu watapata zawadi ya jezi na mpira.
Mashindano hayo,
yalifunguliwa na mechi mbili kati ya shule ya msingi
Nyamwilolelwa na kabusungu, ambapo upande wa
mpira wa miguu shule ya msingi nyamwilolewa iliibuka kidedea kwa bao
6-0 dhidi ya kabusungu huku mpira wa pete nyamwilolelwa ikishinda mabao
30 dhidi ya kabusungu ilioambulia bao 3.
Post a Comment