Mwanamitindo Flavian Matata akiweka shada katika kaburi. |
Baadhi ya wakazi wa Mwanza wakifanya ibada makaburini Igoma Jijini Mwanza |
Baadhi ya wakazi wa Mwanza wakifanya ibada makaburini Igoma Jijini Mwanza |
VILIO na simanzi vimetawala katika makaburi ya Igoma Wilayani
Nyamagana jijini Mwanza wakati ya wa kumbukumbu miaka 19 ya watu
waliopoteza maisha katika ajali mbaya ya kuzama kwa meli ya Mv. Bukoba iliyotokea Mei 21, 1996.
Katika tukio hilo kubwa na la kihistoria la kuzama kwa meli hiyo,
zaidi ya watu 800 walipoteza ambapo kati yao 5 walitambulika na
familia zao na 130 waliweza kuokolewa katika ajali hiyo.
Baadhi ya familia waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo walionekana
wakilia uchungu pale walipolikumbuka tukio hilo kubwa kuwahi kutokea
huku wakiiomba serikali iweze kutambua umuhimu wa kuienzi siku hiyo.
Akizungumza na Ngowi Habari jana wakati wa kumbukumbu miaka 19 Sabina Mrema
mkazi wa kata ya Igoma alisema anasikitiswa kuona serikali kushindwa
kuipa kipambele siku hiyo kwa kuwakumbuka watanzania waliopoteza
maisha katika ajali hiyo.
“Naiomba serikali ione umuhimu wa kuienzi siku hii kwa kuwakumbuka
ndugu zetu waliopoteza maisha katika ajali ya Mv. Bukoba, pia waweze
kuboresha hali ya usafiri wa majini,” alisema Mrema
Kwa upande wake mmoja wa wahanga wa tukio hilo Sterwart Alphonce
alisema hawezi kulisahau tukio la kuzama kwa meli hiyo kwani
alimpoteza mama yake mzazi aliyekuwa akitokea Wilayani Karagwe kuja
Mwanza wakati tukio hilo linatokea.
Alphoncea aliongeza kuwa tukio hilo kuwahi kutokea katika maisha yake
kwani walitumia siku 9 kumpata mpaka pale walipofanikiwa kuitambua
maiti ya mama yake mzazi.
“Siku ya 9 zililetwa maiti 2 na nilitambua moja ni ya mama yangu mzazi
kwa kuona nguo alizokuwa amevaa nilijaribu kuikagua na kukuta
kitambulisho chake na barua ndani ya mfuko baada ya hapo tulimzika na
tulijisikia amani, ” alisema Aphonce.
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela, Rahma Juma, aliye mwakilisha
mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, alisema nivyema vyombo vya
majini kuzingatia sheria za usafiri ili kuepush kutokea kwa ajali za
majini.
Post a Comment