Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza. |
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza amewafuta kazi Mawaziri watatu kufuatia kushindwa kwa jaribio la baadhi la wanajeshi kutaka kupindua nchi ya Burundi wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa msemaji wa Rais Nkurunziza Gervais Abayeho amesema Mawaziri waliotimuliwa ni Waziri wa Ulinzi Pontien Gaciyubenge, Waziri wa Mambo ya Nje Laurent Kavakure pamoja na waziri wa Biashara Marie Nizigiyimana.
Aidha, Bw. Gervais amesema kwamba katiba ya nchi hiyo inampa Rais mamlaka ya kubadilisha watendaji ili kuongeza tija ya utendaji serikalini.
Polisi leo wamefyatua hewani risasi za moto katika kukabiliana na maandamano mapya ambayo yameanza maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Burundi, Bunjumbura.
Makundi ya vijana yaliweka vizuizi barabarani huku wakiimba nyimbo za kumtaka Rais Pierre Nkurunziza abadili msimamo wake wa kutaka kugombea awamu nyingine ya Urais nchini humo.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment