Baadhi ya wanawake wafanyabiashara wa sokoni wakiwa katika kongamano hilo jijini Mwanza |
Baadhi ya wanawake wafanyabiashara wa sokoni wakiiimba kwa furaha katika kongamano hilo jijini Mwanza |
Wafanya biashara wa soko la mkuyuni wakijitambulisha katika kongamano hilo |
Baadhi ya wanawake walioshiriki katika kongamano hilo jijini hapa |
Mkurugenzi Mtendaji wa Equality For Growth(EFG), Jane Magigita akitoa mafunzo kwa wanawake wafanyabiashara walioshiriki kongamano hilo. |
ZAIDI ya wafanyabiashara wanawake 100 mkoani hapa, jana
walipatiwa mafunzo ya kukuboresha ushiriki wao, katika shughuli za
kimaendeleo hususa kumwezesha, kutafakari kwa kina tatizo la umasikini na
kuweka mikakati thabiti ya kukabiliana nalo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la kwanza la
wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania lililofanyika Kwenye ukumbi wa
Mwanza Hoteli , Mkurugenzi wa bodi ya watendaji wa shirika la
Equality for Growth (EFG), Emmanuel Tuju alisema, lengo ni kumwezesha mwanamke
kutumia zaidi mali, nguvu na jitahada ili kujiletea maendeleo na kulinda haki
zao katika umiliki wa mali.
Tuju alisema, sera iliyopo katika sekta isiyo rasmi inawapa
wanawake mwongozo wa serikali unaolenga kuwapa wananchi mwelekeo wa
maendeleo unaohakiki mipango na mikakati inazingatia usawa wa
jinsia kila sekta.
“Kutokana na hili sisi kama Equality For Growth
tumeamua kuleta elimu hii nchi nzima kwa kuanzia mikoa saba ambayo ni Mwanza,
Tanga, Shinyanga, Lindi, Mtwara,Mbeya na Dar es salaam, ili kuhakikisha
mfanyabiashara mwanamke anapata haki ya kumili mali zake”.
Mkurungezi mtendaji wa EFG Jane Magigita alisema, wanawake
wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwepo na sheria inayosimamia
haki zao kutokana na mapungufu makubwa yaliyopo, utashi thabiti wa
viongozi serikalini pamoja na sera kutumika kisiasa zaidi ya maendeleo.
Alisema ili kuinua maendeleo ya sekta hii, viongozi wanapaswa
kutunga sheria na kuzisimamia kwa ajili ya kuboresha
miundombinu pamoja na kutoa fursa, haki sawa kwa wananchi walio katika sekta
hiyo.
Aidha baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambao pia ni
wafanyabiashara wa sokoni walisema, wanakumbana na changamoto mbalimbali
zikiwemo za utozwaji wa ushuru sawa na wafanyabiasha wakubwa.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiasha Soko la
Mkuyuni Veneranda Joseph alisema, Halmashauri imeshindwa kutofautisha
wafanyabiashara wadogo na wakubwa wakati wa kuwatoza ushuru kwani wote
wanalipa kiwango sawa.
Naye Mwenyekiti wa Soko Kuu mkoani Mwanza Ahmed Nchola
alisema, ni vema halmashauri ikatenga eneo husika kwa
wafanyabiashara wanaopanga bidhaa zao chini, kwani wengi wao hawaliipi kodi
kama wanavyolipa wa maduka na meza.
Hatahivyo biashara ndogondogo huzalisha ajira kwa watu
million 2.4 kwa mwaka huku watu 440,000 huingia katika sekta isiyo rasmi
hawa hujumuisha wahitimu wa darasa la saba, waliopunguzwa kazi, wastaafu
na wahitimu kutoka vyuoni.
Post a Comment