![]() |
Add caption |
KLABU ya Simba imekanusha tuhuma za kuuchakachua mkataba wa winga wake, Ramadhani Singano 'Messi' kama anavyodai.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa
wa Msimbazi, Kariakoo jijini hapa jana mchana, Mkuu wa Idara ya Habari
na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara, amesema klabu inatambua mkataba
wa Messi wa miaka mitatu unaomalizika mwakani na si mwaka huu kama
anavyodai winga huyo.
"Habari
hizi ni upotoshwaji, Simba haijachezea mkataba wa Messi kutoka miaka
miwili na kuwa mitatu, Messi ni mchezaji mdogo sana. Naambia hao
mawakala uchwara, waache kumvuruga. Hii ndiyo staili yangu ya leo,"
amesema Manara.
"Tunaomba
TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) walitolee ufafanuzi suala hili badala
ya kukaa kimya kwa sababu taswira ya Simba inachafuka," amesema zaidi
Manara aliyeonekana kufura kwa hasira.
Chanzo: Mpenja Blog
Post a Comment