![]() | |
Rais Kikwete akitia udongo katika kaburi la Mufti Shaaban Bin Simba. |
Rais Jakaya Kikwete jana ameongoza mazishi ya sheikh mkuu wa Tanzania Muft Issa Shaaban Simba aliyefariki jana katika hospitali ya TMJ jijini Dar es salaam siku ya jumatatu.
Aidha, Maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya waisilamu ya nguzo nane mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Shinyanga wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Ally Nassoro Lufunga.
Katika salamu zao za rambirambi baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria mazishi hayo walisema hakika taifa limepoteza kiongozi imara na shupavu ambaye alikuwa kiungo kikuu kati ya madhehebu mbalimbali ya dini na serikali kwa ujumla.
Viongozi wengine wa kitaifa waliopata fursa ya kusindikiza maziko ya sheikh mkuu ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe, Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa, Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye pamoja na viongozi wengine wa dini na serikali.
Post a Comment