Baraza la kikatiba la Hong Kong limeanza kujadili mpango wa mageuzi ya kisiasa kabla ya kupigiwa kura baadaye wiki hii.
Watetezi wa demokrasia wameshutmu hilo kuwa demokrasia ya longo longo.
Tayari mamia ya watetezi hao wamekusanyika nje ya afisi za baraza hilo wakibeba mabango na kutoa maneno ya kutukana baraza hilo.
Lakini wanaoungamkono mpango huo kutoka Beijing wanasema kuwa Hong Kong kwa sasa inahitaji uthabiti na wametoa wito kwa wabunge hao wapitishe pendekezo hilo.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment