![]() |
Wafanyakazi wa uokoaji wakiwa karibu na eneo ilipozama meli |
Waziri wa Usafirishaji wa China
amesema wafanyakazi wa vikosi vya uokoaji wanafanya kila jitihada
kuhakikisha wanawapata watu walionusurika miongoni mwa mamia ya
waliokumbwa na mkasa wa kuzama kwa meli katika mto Yangtze kutokana na
hali mbaya ya hewa.
Watu saba wamethibitika kufa na wengine 14 wamekutwa hai katika meli hiyo iliyokuwa na watu 456.
Ndugu waliojawa na hasira wanalalamikia kukosekana kwa taarifa za uokoaji.
Watu walionusurika ni pamoja na nahodha wa meli na mhandisi mkuu, wote wawili wakiwa katika mahabusu za polisi.
Nahodha amesema meli hiyo ilikumbwa na kimbunga na kuzamishwa chini ya mto katika dakika chache.
Chanzo: BBC Swahili
Post a Comment