![]() |
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe. |
Mpango wa Chama cha ACT-Wazalendo kujiunga UKAWA umeuka kuwa kaa la moto kufuatia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kutamka bayana kuwa hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Aidha, akihojiwa na Waandishi wilayani Kyerwa Mbowe amesema hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kauli ya Mbowe imetolewa baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania. Chama cha ACT-Wazalendo kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.
Katika hatua nyingine, Chama cha ACT-Wazalendo kujiunga na Ukawa huenda ikawa ni ndoto isiyokuwa na majibu huku shauku ya kushirikiana na vyama vingine ikiteketea.
Post a Comment