Mgomo wa mabasi uliotokea hivi karibuni jijini Dares salaam. |
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesitisha nauli mpya zilizotangazwa hivi karibuni ili kuzuia mgogo wa Mabasi uliotangazwa kuanza jana april 29, 2015.
Aidha, Sumatra imesitisha kwa siku 14 utozaji wa nauli mpya za mikoani zilizokuwa zianze leo kufuatia kupata maombi ya rejea kutoka kwa wamiliki wa mabasi ya mikoani kutaka kuangaliwa upya nauli hizo.
Serikali ilitangaza viwango vipya vya nauli Aprili 15 mwaka huu ambavyo vilitarajiwa kuanza leo Aprili 30, mwaka huu kwa kushusha nauli za mabasi ya mikoani.
Akizungumzia maombi ya wamiliki wa mabasi Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu alisema Serikali imetoa wiki mbili kwa Wamiliki wa Mabasi yaendayo mkoani (Taboa), kupeleka hoja yahesabu kwa nini wanasema nauli isishushwe.
Katika hatua nyingine wamiliki wa mabasi ya mikoani wamebainisha kwamba tangu nauli zilipotangazwa kushushwa mafuta na dola vimeendelea kupanda hivyo kushuka kwa nauli kutapelekea wao kupata hasara.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment