Mwenyekiti wa jumuiya , Sheikh Musa Kundecha(kulia). |
Madai ya Madrasa kufungiwa kwa kuhusishwa na kutoa mafunzo ya ugaidi,Taasisi ya Kiislamu nchini imetoa siku 15 kwa Serikali ya Tanzania kuzifungua madrasa zilizofungiwa kabla ya kufanya maandamano nchi nzima kuelekea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Sheikh Musa Kundecha, amesema jeshi hilo limekuwa likiwakamata masheikh na maimamu na kuwapeleka katika vituo vya polisi, na kuwahoji huku wakihusishwa kutoa mafunzo na mazoezi ya kigaidi.
Hatua hiyo inafuatia madrasa zaidi ya 10 kufungwa katika mikoa ya Kilimajaro, Dodoma na Mtwara Kwa tuhuma za kukusanya watoto na kuwafundisha elimu ya dini katika mazingira yasiyofaa.
Masharti mengine waliyoyatoa ni kuachiliwa huru au kwa dhamana masheikh na maimamu waliokamatwa wakituhumiwa kutoa mafunzo na mazoezi ya kigaidi.
Akizungumzia kufungiwa madrasa hizo Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga amesema kuendelea kushikiliwa kwa baadhi ya watu waliokamatwa na kunyimwa dhamana kunatokana na jeshi la Polisi kutojiridhisha au kutokamilika kwa taratibu za dhamana.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment