vote

Burundi yaifunga Mitandao ya kijamii kisa vurugu




Serikali nchini Burundi, imekata mawasiliano ya mitandao ya kijamii kupitia simu za mkononi, ikiwa ni moja ya njia ya kuepusha maandamano ambayo yamekuwa yakipangwa kumpinga Rais Pierre Nkurunziza, kwa kutumia simu.

Inadaiwa kuwa mamia ya waandamanaji wako barabarani kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kwa siku nne wakipinga uamuzi wa Nkurunziza, kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Mitandao ya kijamii iliyofungwa ni Facebook, Whatsapp, Twitter na Tango huku kituo binafsi cha redio nacho kikiwa kimefungwa ikiwa ni harakati za Serikali kuzuia kuenea kwa ujumbe unaohamasisha maandamano.

Inadaiwa kuwa mitandao ya jamii imekuwa ikitumika kuratibu maandamano hayo ambayo ni makubwa zaidi nchini Burundi, tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005.

African Public Rasio, maarufu kama ‘Sauti ya Wasio na Sauti’, ni moja ya vituo vitatu vya redio ambavyo matangazo yake ya moja kwa moja yamesitishwa, kwa kile ilichodawa na Serikali kuwa vinavuruga amani.

Chanzo: Hivi Sasa
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog