Kajala atishiwa maisha, apewa siku tano za kuishi
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja hivi karibuni amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kufuatwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake na kutoa onyo kuwa wanampa siku tano tu za kuishi.
Inadaiwa kuwa watu hao wapatao watatu walitinga nyumbani hapo usiku huo mnene huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Rav 4, milango mitano rangi ya bluu ya kuiva na kumkuta mlinzi getini ambapo walimuuliza kama Kajala yupo, na mlinzi kuwadanganya kwamba hayupo.
Inadaiwa kuwa watu hao walisema kuwa Kajala, aambiwe kuwa kuna watu walifika, wamempa siku tano za kuishi na kwamba wao wametumwa na mtu wa karibu na Kajala, lakini hawakumtaja kwa jina.
Kwa mujibu wa Kajala, amesema kuwa hakuogopa japokuwa habari hizo zimemchanganya kupita kiasi, na kujiuliza maswali mengi kuwa ni mtu gani wa karibu ambaye anampa vitisho.
Ameongeza kuwa mtu huyo sio mtu wa karibu bali ni adui yake na kudai kuwa tayari ameshatoa taarifa kituo cha Polisi Kijitonyama jijini Dar es Salaam, kwa tahadhari.
Chanzo: Hivi Sasa
Labels:
habari
Post a Comment