vote

Mabasi ya Abiria kuanza tena siku 7 za Mgomo


Hali ilivyokuwa wakati wa mgomo wa Madereva kituo kikuu cha mabasi Ubungo.

Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani Wamesema kuwa watagoma  kusafirisha abiria nchi nzima kwa madai ya SUMATRA kushusha nauli huku bei za mafuta zikipanda.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana  katika kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani , Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema SUMATRA ilikurupuka  kushusha nauli bila kufanya mchanganuo na kuitaka mamlaka hiyo kurejesha bei za nauli kama awali.

Wamiliki hao wameafikiana kuwa  ikiwa SUMATRA hawatatoa  majibu mapema kuanzia  Aprili 29 mwaka huu hawatokata tiketi kwa wasafiri na yeyote atakayetoa gari lake kufanya biashara kabla hawajapata muafaka kutoka SUMATRA watamchukulia hatua za kisheria.

Hata hivyo wamiliki hao  wameitaka serikali kurudisha viwango vya nauli za mabasi ya mikoani kwenye hali yake ya kawaida iliyokuwepo miezi michache iliyopita kwasababu bei ya mafuta imerudi juu, baada ya kushuka kwa kisingizio cha bei ya mafuta kushuka.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog