Mfalme Zulu Goodwill Zwelithini |
Inadaiwa kuwa mfalme wa Kizulu, Goodwill Zwelithini, amekanusha kuwa kauli yake siyo sababu iliyopelekea raia wa kigeni kushambuliwa na kuuawa.
Tujikumbushe,
Wiki mbili zilizopita raia wa Afrika Kusini, walizusha ghasia kubwa dhidi ya wageni waishio nchini humo kwa kigezo cha kwamba wanachukua kazi zao ambapo walivamia maduka ya wageni na kupora mali zilizomo na kusababisha mamia ya raia wakigeni kuondoka nchini.
Kwa mujibu wa msemaji wa baraza hilo David Mark, amesema kuwa unyama waliofanyiwa raia wa kigeni nchini Afrika Kusini, haukubaliki hata kidogo na kuomba mfalme Goodwill, afikishwe mahakamani kwa uchochezi wake.
Ameongeza kuwa haiwezekani kwa kiongozi mkuu kusimama katika hadhara na kusema kuwa raia wa kigeni wanapaswa kuondoka ambapo matamshi hayo ndiyo yalichochea chuki kwa raia hao.
Chanzo: Hivi Sasa
Post a Comment