Lowassa afunga mahesabu ya Wadhamini Morogoro
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amehitimisha safari ya kusaka wadhamini katika mikoa 15 ya Tanzania bara na mitatu ya visiwani Zanzibar.
Akiwa Mkoani Morogoro Lowassa amepata wanaccm 104,038 waliojitokeza kumdhamini katika safari yake ya matumaini aliyoa ianza mara baada ya kutangaza nia ya kugombea urais uwanja wa sheikh Abeid Karume jijini Arusha may 29 maka huu.
Lowassa pamoja na watia nia wengine CCM wanatakiwa kurejesha fomu za urais makao ya Makuu ya CCM mkoani Dodoma wiki hii huku mwisho wa kurejesha fomu hizo ikiwa ni julai 3,2015.
Baada ya kurejesha fomu watasubiri matokeo ya mchujo utaofanywa na kamatia Kuu CCM itakayoketi na kuanza zoezi a uchujaji.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na chama hicho inaonesha kuwa vikao vya uchujaji vitakuwa kama ifuatvyo,
Kamati ya usalama na Maadili Zanzibar 4/7/2015
Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya Taifa 5/7/2015
Kamati ya Usalama na Maadili Taifa 8/7/ 2015
Kamati ya Halmashauri kuu ya Taifa 9/7/2015
Halmashauri kuu ya Taifa 10/7/2015
Mkutano mkuu wa Taifa 11-12/7/2015
Chanzo:Hivi Sasa
Labels:
habari
Post a Comment