Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe |
Kiongozi mkuu wa Alliance for Change and Transparency (ACT - Wazalendo), Zitto Kabwe,
amewaomba Watanzania kupima sera na matendo ya viongozi wa chama hicho
kujiridhisha kwamba kinafaa kuwaletea maendeleo ya kweli.
Zitto
alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara mjini Musoma, Mara, hivi
karibuni, akisema wananchi wana hiari ya kujiunga na chama chochote cha siasa
wanachoona kinawafaa.
Akifafanua
zaidi, Zitto aliwaomba wananchi kumpima vitendo vyake kutokana na uvumi
unaosambazwa na baadhi ya watu kwamba ni msaliti wa kisiasa.
Alisema
wanasiasa kutofautiana ni jambo la kawaida, hasa mtu anapopigania masilahi ya
wananchi katika jumuiya ya wanasiasa wengi.
Zitto
umefika wakati wa kufanya siasa za maendeleo badala ya kutumia majukwaa ya
siasa kumtukana mtu au chama kingine.
“Kinachotakiwa
ni mwanasiasa kusimama jukwaani na kuwaeleza wananchi atakachowafanyia iwapo
watawachagua na siyo kutukanana kwani wananchi wana kiu na maendeleo na siyo
kutukanana matusi,” alisema Zitto na kuongeza:
“Hivi
ukigombana na mke wako ndani halafu ukaenda kijiweni kuwaeleza wenzako kuwa
tumegombana na mke wangu ndani na ukawaeleza sababu za kugombana ni nani
atakayeonekana mjinga, mke wako au wewe uliyeenda kuwaeleza?”
Mwenyekiti
wa chama hicho Taifa, Anna Mghwirim, alisema siasa ni maisha, hivyo wanasiasa
wanaochezea maisha ya wananchi hawastahili kukabidhiwa uongozi wa umma.
Alisema
chama hicho kimekuja na misingi thabiti ya kuinusuru nchi inayolemewa na mzigo
mkubwa, hasa wa ukosefu wa ajira kwa vijana wengi.
“Taifa
kwanza leo na kesho ili kurudisha misingi yote iliyokuwepo ambayo kwa
sasa haitumiki, lengo ni kurudisha matumaini kwa wananchi,” alisema.
Post a Comment