vote

Escrow yazidi kumtesa Ngeleja jimboni jimboni kwake

 
Mbunge wa jimbo la Sengerema, Wilium Ngeleja

MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), juzi alikabiliwa na hali
mgumu ya kujibu maswali kutoka kwa wakazi wa jimbo hilo kuhusu kashfa
ya kujipatia Sh milioni 40 ambazo ni sehemu ya  Sh zaidi ya bilioni
300 zinazodaiwa kuchotwa kinyemela kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.



Baadhi ya wananchi hao walitaka kujua matumizi ya fedha hizo
alizopokea kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and
Marketing Limited, James Rugemalira.

Mmoja wa wananchi hao, James John, aliuliza “Mheshimiwa wakati
unapanda jukwaani umesema huwezi kubali ukweli kuwa uongo na uongo
kuwa ukweli, nauliza; kwenye suala la Escrow ulionekana kuwa mtuhumiwa
katika kamati ya maadili na ukafukuzwa kwenye NEC na Kamati ya Katiba
na Sheria.

“Wakati unahojiwa na Kamati ya Maadili hizo fedha ulizopokea ulitoa
vielelezo kwamba ulizipeleka makanisani na miskitini huko Dar es
Salaam; swali langu ni je, fedha iliyobaki italisaidiaje jimbo la
Sengerema na ututajie hata mradi mmoja uliotumia fedha hizo?” 

Swali hilo lilimfanya Ngeleja kutumia muda wa saa 1:05 kulitolea
ufafanuzi mbele ya wananchi waliokaa kimya kumsikiliza huku baadhi yao
wakitoa minong'ono iliyoonyesha kutoridhishwa na majibu yake.

Hata hivyo, Ngeleja alitumia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba fedha
hizo siyo za Serikali, kujisafisha kwa wananchi hao katika mkutano wa
hadhara mjini hapa.

Ngeleja aliwafafanulia wananchi mchakato ulivyofanyika hadi wao
kubainika kuhusishwa kwenye sakata hilo.

“Ukisikia jambo linapelekwa bungeni halipelekwi kwa ujumla, suala la
fedha lilipelekwa kwenye kamati ya Zitto kabla hajafukuzwa na wenzake.

Ngeleja alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
kazi yake aliyopewa alimaliza na kupitia kauli ya waziri mkuu, alileta
taarifa hiyo bungeni kupitia kamati ya Zitto na kwamba haikuonyesha
kuwataja kuhusika na wizi wa fedha hizo.

“Hapa naomba mnisikilize kwa makini, huyu CAG hakumtaja mtu yeyote
kwamba wewe Profesa Tibaijuka, sijui Andrew Chenge, wewe Ngeleja
mbunge wa Sengerema na wewe Askofu Kilaini. Hakumtaja mtu yeyote
kwamba alipata fedha kinyume na utaratibu, isipokuwa lilipofika kwenye
kamati ya bunge lilikuzwa,” alisema Ngeleja.

Alidai kwamba kilichotokea pale bungeni muda wote wa mjadala
Watanzania waliaminishwa kwa mambo mawili kwamba zile fedha zilikuwa
zimetunzwa Benki Kuu (Bot), zilipaswa zirudi kwenye kampuni ya IPTL,
zilikuwa fedha za umma kama kamati ya Zitto ilivyodai.

Ngeleja alisema,CAG hakusema hivyo na alichokisema katika fedha hizo
labda kulikuwa na kodi ambayo ilipaswa kulipa kwa sababu Tanesco
ilitakiwa kuilipa kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Alisema hoja ya pili kamati ilikuwa kwamba inawezekana katika fedha
hizo zilichukuliwa kutoka Escrow zikaenda kwa PAP na SingaSinga, wao
kamati walisema zilikuwa fedha za umma ili hali hazikuwa fedha za
umma.

Kwa upande mwingine, wananchi hao walitumia nafasi hiyo pia kumhoji
mbunge huyo sababu ya kuchelewa kutekeleza ahadi ya kuwatatulia kero
ya uhaba wa maji inayowakabili kwa miaka mingi, ambapo aliwajibu
kwamba juhudi za kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo linaendelea.

Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog