vote

Jeshi la Wananchi lazua kizaa zaa songea

Jeshi la Wananchi JWTZ mkoani Ruvuma.



Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wilayani Songea jana limezua kizaa zaa kwa wananchi kufuatia kuvamia mitaani, maofisini (serikali na binafsi) makanisani na misikitini wakiwa na silaha huku magari yao yakiranda kila kona na kuanza upekuzi  kwa watu wote walokutana nao huku wakidai kuonyeshwa vitambulisho.

Aidha,indaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mjini hapo waliamua kujifungia ndani huku wengine wakisema kwamba jeshi hilo linawasaka  magaidi waliovamia katika mji wa Songea kutoka na jeshi hilo kutowafahamisha wananchi nini hasa dhumuni la msako huo.

Kwa mujibu wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alipoulizwa alisema zoezi hilo ni la kawaida  huku akiwataka wakazi wa mjini songea  kuwa na amani na waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida.

Naye  Brigedia Jenerali wa Kamandi ya Kusini, John Chacha alisema hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa wanajeshi hao na kuongeza kuwa  jeshi hilo  hufanya mafunzo mbalimbali ya kujiimarisha ikiwamo ya kulinda miji, maporini na mengineyo.

Chanzo: hivi sasa
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog