vote

Utata kifo cha mtendaji kata


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi

OFISA Mtendaji wa Kata ya Kyanyari wilayani Butiama, Alfred Kitambara
(58), amekutwa amefariki dunia katika mazingira yaliyojaa utata katika
kitongoji cha Kibisa,kijiji cha Nyamisisi wilayani hapa kwenye
barabara kuu ya Mwanza-Musoma huku kichwa chake kikiwa na majeraha
makubwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi, aliliambia gazeti
hili mkoani hapa jana kwamba mwili wa Kitambara uliokotwa na wapita
njia saa mbili usiku wa kuamkia jana kando ya barabara hiyo.

Kamanda Kalangi alisema majeraha makubwa kichwani na katika mguu wake
wa kushoto wa marehemu huyo yanaashiria kuwa huenda aligongwa na gari
lisilojulikana na mwili wake kutelekezwa katika eneo hilo.

Awali, asubuhi ya siku hiyo mtendaji huyo alikwenda kazini kama
kawaida na ilipofika jioni alionekana katika baa moja ya kuuza pombe
katika kijiji cha Mwibagi na baadaye kwa kutumia usafiri wa pikipiki
yake kurejea nyumbani kwake Kiabakari ambako hata hivyo hakufika
kutokana na kukutwa na mauti hayo.

Kwa mujibu wa Kamanda Kalangi, pikipiki hiyo ya ofisa mtendaji huyo wa
kata ilikuwa imeegeshwa upande mwingine wa barabara hiyo ikiwa
haijaharibika.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema kabla ya kufikwa na mauti hayo,
mtendaji huyo alimpigia simu mke wake saa 1:30 usiku na kumweleza
kwamba amepotea njia ya kurudi nyumbani hali iliyosababisha mwenzi
wake huyo kukodi pikipiki na kumfuatilia barabarani, lakini alipofika
eneo la Kibisa alikuta kundi kubwa la wananchi waliomueleza kwamba
wamemwokota mume wake huyo akiwa amefariki dunia

Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog