Wafanyakazi
wa umma na sekta binafsi jijini Mwanza wameshauriwa kujiandikisha kwa wingi
kwenye daftari la wapigakura ili waweze kuwachagua viongozi bora katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Chama cha Wafanyakazi
Tanzania (Tucta), Yusuph Simbaulanga, alisema kura ni nyenzo muhimu inayoweza kuepusha
malalamiko yasiyo ya lazima yanayoweza kujitokeza baada ya uchaguzi.
“Idadi
ya watu wanaojiandikisha imeongezeka, hivyo kwa fursa hii ni vyema pia
wafanyakazi kujiandikisha kwa wingi kwani wengi ni vijana wanaofanya kazi katika
sekta binafsi na za umma,” alisema Simbaulanga.
Aidha,
alisema kujiandikisha kwa wafanyakazi kutawafanya kuoana thamani ya kura zo
katika kufanya uamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba
mwaka huu.
“Kupitia
sanduku la kura mfanyakazi ataweza kujikomboa kwa kuchagua viongozi watakaoleta
tija kwenye utendaji, lakini pia kuboresha maslahi yao,” aliongeza Simbaulanga.
Alitumia
nafasi hiyo pia kuwahimiza
wafanyakazi
kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mwaka huu
itakayofanyika kitaifa jijini Mwanza ili kushiriki pia kupima afya zao kuhusu
magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na ukimwi, ambapo wataalamu wa afya
watatoa vipimo hivyo bila malipo.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo yanayoratibiwa na chama cha wafanyakzi wa
migodini, nishati na ujenzi (Tamico) chini ya Tucta ni Rais Jakaya Kikwete.
Post a Comment