vote

Kero za Wafanyabiashara soko la Mabibo zatua kwa Makonda.


Mkuu wa Wilaya Kinondoni Paul Makonda akiwahutubia wafanya biashara soko la ndizi mabibo.


Kero mbalimbali zinazowakabili wafanya biashara katika soko la Ndizi la Mabibo Kinondoni jijini Dar es salaam hatimaye zimetua kwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda aliyetembelea soko hilo leo.

Kwa mujibu  wa  wafanyabiashara katika soko la mabibo takribani 10000 wametaja kero zinazowakabili sokoni  hapo kuwa ni hawajui hatma ya biashara yao Sokoni hapo kwa kuwa  eneo wanalofanyia biashara sio rasmi kwajili ya soko  ni Mali ya Kiwanda cha Urafiki, Kutokana na kutokutambulika kwa eneo hilo kama eneo la soko kunawanyima fursa mbalimbali ikiwemo Mikopo kwa kuwa eneo hilo halitambuliki, Miundombinu ya Soko haifai kabisa hali inayosababishwa kutokutambulika kama sehemu ya soko pamoja na wafanyabiashara  hao kutojua  hatma ya maisha yao.

Akizungumza mara baada ya kukagua soko hilo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda amesema  amepokea kwa mikono Miwili Kilio chao  na kuahidi  kuwa atalifanyaia kazi kwa haraka kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za Maamuzi na Mapema atawajibu.

Ameongeza kuwa ni  Ngumu sana kwake  kutoa ahadi ambayo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa Eneo hilo ni Mali ya Kiwanda cha urafiki na kiwanda kimebinafsishwa ni ngumu kuaahid kama watalipata eneo hilo kwajili ya Soko bila kujua Mipango ya Kiwanda kuhusu eneo hilo.

Kwa upande mwingine Makonda amesema kwenye ofisi yake kila siku ya Jumanne ni  siku ya Kumwona Mkuu wa Wilaya kwa  hiyo ametoa rai wa wakazi wote wa kinondoni wenye matatizo Mbalimbali Kufika ofisini kwake kila Jumanne kumwona.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog