![]() |
Raia wa Ehiopia wakichinjwa na wanamgambo wa Islamic state. |
Nchi ya Ethiopia imeanza rasmi siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na wanamgambo wa kundi la Islamic State nchini Libya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali nchini humo imebainisha kwamba bendera zitapepea nusu mlingoti wakati nalo bunge la nchi hiyo likikutana kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya ishirini.
Msemaji wa serikali Redwan Hussein, alisema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani ulaya.
Mungano wa Afrika ambao una makao yake makuu nchini Ethiopia umelaani mauaji hayo na kusema kuwa utafanya mikakati ya kuhakikisha kuwepo usalama nchini Libya.
Post a Comment