vote

Lowassa atoa ya moyoni mauaji ya Albino Tanzania


Mh, Edward Lowassa
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa jana ametembea umbali wa kilomita tano kwa miguu kwenye matembezi ya kupinga mauaji  ya albino  nchini.Matembezi hayo yalianzia Uwanja wa Taifa wilayani Temeke mpaka viwanja vya TCC Chan’gombe huku yakitumia dakika 25.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tanzania wameiambia hivisasa blog kwamba katika matembezi hayo Lowassa  amewaondoa hofu wananchi  na kudhihirisha    kuwa afya yake iko safi kutokana na kudaiwa kuwa na matatizo ya afya huku wengine wakisema  hawezi kuhimili mikimiki ya kampeni na shughuli nyingine zinazohitaji nguvu.

Matembezi hayo yalianzia barabara ya Mandela, Kilwa kupitia Temeke Mwisho, Wiles, Temeke Hospitali, Chang’ombe Polisi, Kiwanda cha Bia cha Serengeti na kuhitimishiwa viwanja vya TCC.

Akizungumza baada ya kuhitimisha matembezi hayo yaliyoandaliwa na kikundi cha Temeke Family Sport Club Lowassa ameitaka  Serikali kuongeza jitihada katika uhamasishaji na kupinga mauaji hayo.

Katika hatua nyingine Lowassa ameitaka jamii kutambua kuwa  albino ni sawa na watu wengine na wasitengwe kwa sababu nao wana haki ya kuishi kama watu wengine.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog