vote

Wakimbizi 152,572 wapewa uraia Tanzania


Baadhi ya wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania.

Wakimbizi kutoka nchini Burundi  nchini  waliopo Tanzania zaidi ya 152,572 walioingia nchini h tangu mwaka 1972, hatimaye  wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania. na kuwa huru kuishi.

Akizungumzia suala hilo  msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Isaack Nantanga amesema hatua ya Tanzania kuwapa uraia wakimbizi hao ni kutokana na hiyari yao na kwamba serikali ya Tanzania ilishauriana na Burundi na hatimaye kukubaliana wapatiwe uraia wanaotaka wa kuwa Watanzania.

Wakimbizi hao walikuwa wameomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na waziri wa mambo ya ndani mwaka 2010, sasa ni halali kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za udiwani na ubunge.

Nye mkuu wa makazi ya Mishamo, Frederick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka 2014 katika makazi ya Katumba mkoani Katavi magharibi mwa Tanzania ambako watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye kuhamia katika makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania ambako wakimbizi 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog