Rais Pierre Nkurunziza. |
Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Kuwa mujibu wa vituo vya redio nchini humo, Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi .
Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse, alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.
Hatua hiyo inafuata kuibuka machafuko nchini humo ya kumpinga Nkurunziza kuwania muhula mwingine wa urais suala ambalo ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Hata hivyo Serikali ya Tanzania imebainisha kupokea wakimbizi takribani 2000 huku wengine wamiminika mpakani mwa Tanzania kutokana na kukimbia mgogoro huo nchini Burundi.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment