Baadhi ya Waasi wa ADF. |
Askari wawili wa Tanzania waliokuwa kwenye kikosi cha usalama cha MONUSCO wameuawa baada kushambuliwa na watu wenye silaha katika maeneo ya Kivu ya Mashariki.
Aidha, katika shambulizi hilo lilitokea jana wanajeshi 13 wamejeruhiwa na waasi hao huku wanajeshi wanne wakiwa hawajulikani walipo.
Akizungumzia tukio hilo msemaji wa MONUSCO, Felix Basse amevieleza vyombo vya habari kuwa shambulizi hilo la kushtukiza limefanywa na waasi hao ikiwa ni siku moja kupita baada ya jeshi la Congo kuwau waasi 16 wa ADF.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment