Baadhi ya wanafunzi wa mchezo wa judo katika chuo cha Shotokan Karate wakifanya mazoezi jana, katika uwanja wao uliopo Igoma Jijini Mwanza. |
JAMII imetakiwa kuuchukulia mchezo wa Judo (Karate) kama
michezo mingine ya kuimarisha viungo na kuondokana na dhana iliyopo ya kuwa
mchezo huo ni ugaidi.
Akizungumza na BINGWA jana, Mwalimu wa Judo katika chuo cha
Shotokan Karate, Amri Khasani alisema kuwa jamii inatakiwa kuelewa kuwa mchezo
wa Judo ni sawa na michezo mingine ya kuimarisha Afya.
“Mchezo huu wa Judo kwa hapa Mwanza hauna kipaumbele sana
kutokana na jamii kuuchukulia tofauti, lakini nikuhakikishie kuwa hakuna mchezo
mzuri kama huu kwa kuwa unaimarisha mwili kwa asilimia kubwa” alisema Khasani.
Kwa upande wake Nasoro Suleimani anayecheza Judo alisema
anashangazwa na vijana wengi wa Mwanza kwa kutokujiunga na Mchezo huo kwa kuwa
unawaepusha na mambo mengi ya kihuni.
“Mchezo huu nimeucheza tangu mwaka 1977, nakumbuka siku moja
nimempeleka mke wangu Hospitali kujifungua usiku wakati narudi nikavamiwa na
wezi lakini nikawakabili na kumkamata mmoja wao, kama sikuwa na mazoezi
wangenimaliza” alisema Suleiman.
Hata hivyo Suleiman aliitaka Serikali kutoa kipaumbele kwa
mchezo huo kwa kuwa unaweza kuisadia kuwa na vijana wengi walio imara.
Post a Comment