Moja ya kituo cha kupigia kura cha kwenye baa nchini Uingereza. |
Mamilioni ya watu watakuwa wakipiga kura katika uchaguzi mkuu wa Uingereza leo Alhamisi Vituo vingi vya kupigia kura viko katika majengo ya shule, kumbi za vituo vya kijamii na kwenye kumbi za parokia, lakini migahawa, maeneo ya kufua na kunyosha nguo na basi la shule pia vitatumika kama vituo vya kupigia kura.
Vituo vya kupigia kura karibu 50,000 nchini kote vitafunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za Uingereza.
Jumla ya wabunge 650 watachaguliwa kuingia bunge la nchi hiyo, kukiwa na watu karibu milioni 50 waliojiandikisha kupiga kura.
Kama ilivyo kwa uchaguzi mkuu, kuna viti zaidi ya 9,000 vya madiwani vinavyogombewa katika serikali za mitaa 279.
Mameya pia watachaguliwa katika miji ya Bedford, Copeland, Leicester, Mansfield, Middlesbrough na Torbay.
Hii ina maana kuwa karibu kila mpiga kura wa England, ukiondolewa mji wa London ambako hakuna uchaguzi wa serikali za mitaa, atapewa karatasi mbili za kupigia kura watakapofika katika kituo cha uchaguzi.
Chanzo: Hivi sasa
Post a Comment