Wananchi mbalimbali jijini Dar es salaam wamepinga vikali suala la mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kugomea kushusha nauli za daladala kufuatia nauli za mabasi ya mikoani kutangazwa kuwa zimeshuka siku ya jana.
Bei hizo mpya za mabasi ya masafa marefu zimeshuka kwa asilimia kadhaa kulingana na urefu wa safari kwa mfano, mabasi makubwa yanayofanya safari za kwenda mikoani pekee kwa asilimia 7.8 ambapo kwa mfano nauli ya kutoka Dar es salaam Arusha mwanzo ilikuwa elfu 22700 na kwa sasa itakuwa 21000.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Gilliard Ngewe amesema uamuzi wa kushusha nauli hizo unafuatia mamlaka hiyo kufanya utaratibu wa kupitia kanuni kwa kuwashirkisha wadau mbalimbali ikiwemo watoa huduma ili kutoa maoni kutokana na ongezeko la Msongamano wa magari mjini.
Wakizungumza na Mwandishi wa Habari wa Mtandao wa Hivisasa baadhi ya wananchi ambao pia ni watuamiaji wa daladala wamesema kwamba kutoshuka kwa nauli ni dhahiri kuwa serikali inawabeba wamiliki wa vyombo usafiri ili wapate faida kubwa huku wananchi wakiteseka kwa ugumu wa maisha.
Mwanaidi Shaban mkazi wa Mabwepande amesema kwamba serikali ina wasomi lakini wasomi hao ni bure kabisa kwani mafuta yameshuka bei kipindi kirefu wao wanatangaza kushuka bei jana, hata hivyo bei hizo zinaonekana zipo kisiasa zaidi kwani hazina tija kabisa kwa wananchi.
Mwingine ni Amos Jumanne mkazi wa Mbagala jijini Dares salaam amesema kwamba siku hizi daladala zimekuwa zikijipangia nauli hasa majira ya asubuhi na usiku hakuna hatua wanazo chukuliwa, leo hii bei zinabaki vile vile huku mafuta katika soko la dunia yanazidi kushuka serikali haioni kuwa haiwatendei haki wananchi.
+ comments + 1 comments
Hili suala la kutoshuka Kwa nauli za daladala hata kama Mafuta yakishuka bei katika soko la dunia hii kimtazamo inawezekana wamiliki wa Vyombo hivyo vya usafirishaji wapo ndani ya mamlaka hiyo na ndio maana inakuwa ngumu kupata muafaka mzuri wa kuwasaidia wananchi unafuu wa nauli ukizingitia asilimia kubwa wanao panda daladala ni jamii ya watu wa hali ya chini nikimaaniha wenye vipato vidogo.
Post a Comment