vote

UNHCR yaingilia kati Kenya kuifunga kambi ya Dadaab




Kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo karibu na mpaka wa Somalia.

Shirika la umoja wa mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeingilia kati mpango wa serikali ya Kenya kutaka kuifunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo karibu na mpaka wake wa Somalia.

Shirika hilo limeitaka serikali ya Kenya kufikiria upya kauli hilo ya kuwatimua  wakimbizi na kufunga kambi hiyo katika kipindi cha miezi tatu ijayo.

Hatua hiyo inafuatia Serikali ya Kenya kutoa amri hiyo punde baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab kuwaua wanafunzi wakristu takriban 150 katika chuo kikuu cha Garissa mapema mwezi huu.

Makamu wa Rais William Ruto alitangaza kuwa angetaka wakimbizi hao warejeshwe makwao na kambi hiyo ya Dadaab ifungwe. Kambi hiyo yenye wakimbizi takriban nusu milioni ndio kubwa zaidi duniani ikiwa na asilimia kubwa ya wakimbizi kutoka Somalia.

Serikali ya Kenya imesema ina  ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa asilimia kubwa ya mashambulizi yanayotekelezwa nchini Kenya na kundi la waislamu la Al Shabaab yanapangiwa katika kambi hiyo ya Dadaab.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog