Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye.
Chama cha Mapinduzi CCM kimefunguka kuhusiana na mashinikizo yanayotolewa na baadhi ya watu wakikitaka chama hicho kitangaze haraka ratiba ya uteuzi wa wagombea wake kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Kauli ya Nape imekuja baada ya baadhi ya makada wa chama hicho kuhoji inakuwaje CCM kinachelewa kutoa ratiba ya mchakato wa uchaguzi, wakati muda unasonga pamoja na kubakia miezi kadhaa kufikia muda wa kampeni pamoja na uchaguzi mkuu.
Kwa mujibu wa katibu wa itikadi na uenezi CCM Nape Nnauye amesema vikao vya chama ndivyo vitakavyoamua mchakato huo uanze lini, lakini CCM haina historia ya kuwahi wala kuchelewa.
Amesisitiza kuwa CCM mara nyingi huandaa ratiba yake kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec). Hao wanaotaka kuharakisha mambo wajaribu kupitia mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010, CCM ilitangaza uteuzi muda gani.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka ndani ya chama hicho,vimebainisha kuwa huenda chama hicho kikatangaza ratiba ya uteuzi wa wagombea urais ifikapo mwezi juni mwaka huu. Huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka 2015.
Post a Comment