vote

Jeshi la Polisi nchini lawaonya madereva waendao mwendokasi.

 



Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Johansen Kahatano

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani limewaonya wamiliki wa mabasi ya abiria kuacha tabia ya kuwaamuru madereva wao kwenda mwendo wa kasi na kwamba halitasita kuchukua hatua dhidi ya wamiliki hao.
Akihojiwa Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Johansen Kahatano, kuwa kuna umuhimu wa madereva wote wa vyombo vya moto nchini kwenda kusoma kwani hatua hiyo itawapa umahiri wa kazi yao.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza kiwango cha tatizo la ajali za barabarani zinazotokea takribani kila siku hapa nchini.
Ameongeza kuwa kuna haja ya madereva kufuata sheria za barabara hasa katika kuangalia mwendokasi ambapo ndio chanzo cha ajali nyingi za barabarani
Share this article :

Post a Comment

 
Support : GUDMUSICS BLOG | Gm Template | Gm Template
Copyright © 2015. NGOWI HABARII - All Rights Reserved
Template Created by 0756494700 Published by GM Template
Proudly powered by gudmusics blog