Chama cha Upinzani kimezidi kuchanja mbuga nchini Nigeria kufuatia kupata ushindi mkubwa wa majimbo 19 kati ya 29 katika matokeo ya hivi punde yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi INEC.
Awali INEC ilikuwa imethibitisha kuwa chama cha rais mteule The All Progressives Congress (APC) kilikuwa kimetwaa miji mikuu ya Lagos Kaduna na Katsina.
Matokeo haya ya hivi punde ni dhihirisho kuwa raia wa Nigeria walipigia Kura kiongozi wa upinzani Jenerali mtaafu Muhammadu Buhari.
Ushindi huo ni dhidirisho ya kuwa chama kinachoondoka madarakani cha Rais Goodluck Jonathan PDP kimepata kichapo chake kikubwa zaidi tangu kukamilika kwa utawala wa kijeshi mwaka wa 1999.
Ushindi huu wa majimbo zaidi unaiongezea pondo serikali mpya haswa baada ya kutwaa ushindi mkubwa dhidi ya Rais Goodluck Jonathan.
Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari anatarajiwa kuapishwa rasmi kama rais wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika mwishoni mwa mwezi Mei.
Post a Comment